Malezi Talk
Kipindi #1 cha malezi ya familia, watoto na wazazi.
Malezi ni jukumu maalumu la muda mrefu linalomdai mzazi au mlezi kumsaidia mtoto/kijana kuyamudu, kuyakabili maisha na mazingira yake kwa ujumla.
Sisi wana St. Josephs' kama sehemu ya walezi, tunao lea vijana shuleni, tumeamua kutoa mchango katika kuwakumbusha wazazi na walezi wenzetu baadhi ya mambo tunayoamini ni ya msingi kabisa katika kulea.
Yaliyomo katika kipindi cha malezi.
Familia
Familia ndio nguzo ya jamii, familia ikitetereka jamii pia itatetereka. Tutaongelea namna tutakavyoweza kujenga familia bora yenye, upendo, heshima na amani.
Wazazi
Tunaamini wazazi ndio wawekezaji wakuu kwenye malezi ya awali ambayo ni miaka 0-8 ya mtoto. Muda huo ndio msingi wa kumuandaa mtoto kua kijana bora kwenye jamii.
Watoto
Watoto ni taifa la kesho, ndio baba na mama wa vizazi vijavyo. Ni maadili gani na misingi gani inapaswa ijengwe ndani yao ili waweze kufanikiwa kwenye maisha?
Walezi
Sambamba na wazazi, watu watakao mlea mtoto wana nafasi kubwa ya kushawishi tabia na mienendo ya mtoto kadri anavyokua. Ni muhimu kuelewa ushawishi huu.
Sr. Theodora Faustine
Mkuu wa Shule
St. Joseph's Cathedral High School
Sr. Theodora ni Mtawa wa Shirika la Dada Wadogo wa Mtakatifu Fransisko wa Asizi -Jimbo Kuu la Dsm. Mkuu wa Shuke mwanzilishi wa St. Joseph’s Cathedral High School.
Ni shule ya kidato cha Tano na Sita inayochukua vijana wa kiume na Kike wanaotoka mazingira mbalimbali na Imani mabo mbali.
Sr. Theodora amekuwa Mkuu wa Shule tangu kuanzishwa kwa shule 2010 hadi leo 2023. Ana uzoefu wa kulea vijana wa miaka kati ya 15 - 20 kwa zaidi ya miaka 10.